Mwanaume afanya mazishi ya kumkejeli mkewe aliye hai
Mwanaume
mmoja katika kijiji cha Emakhwale, kaunti ya Kakamega nchini Kenya amewaacha
wakazi wa eneo hilo na mshangao baada ya kufanya mazishi ya kejeli ya mkewe
waliyeachana naye.
Jack
Shiundu, 32 na mkewe Lydia Masakwe, walinunua kipande cha ardhi mwaka mmoja
uliopita na walikuwa wakiishi pamoja.
Shiundu
anadaiwa kuchimba shimo na kufukia jeneza hilo dogo na kulifunika kwa nguo na
picha za mkewe Masakwe ambaye bado yuko hai.
Kulingana
na TV47, jeneza hilo liligunduliwa na mkulima mmoja.
Alipoichimba,
pia alipata kile kilichoonekana kama vipande vya nywele za binadamu ndani ya
jeneza.
Hata
hivyo, familia ya Masakwe sasa imewataka polisi kumkamata mshukiwa mbaye
ameingia mafichoni.
Katika
kisa cha awali tuliliripoti kwamba polisi katika kaunti ya Embu
wanachunguza kisa ambapo mzee wa miaka 70 anadaiwa kumdunga kisu mkewe hadi
kufa baada ya kutofautiana kuhusu KSh 6000. Marehemu mwenye umri wa miaka 42,
aliripotiwa kutoweka na pesa walizolipwa baada ya kuuza mbuzi.
Akithibitisha
kisa hicho, kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Embu Mashariki Benjamin Muhia
alisema baada ya kutoweka, mwanamke huyo alirejea nyumbani akiwa mlevi bila
senti hata moja.
Chifu
wa kijiji cha Thau Daniel Ndwiga alisema alipata taarifa ya tukio hilo mwendo
wa saa kumi na mbili jioni na alipofika eneo la tukio aliwakuta majirani
waliokuwa na hasira wakipanga kumuua mshukiwa.
Majirani
wa wanandoa hao walisema walikuwa na mizozo ya nara kwa mara na hata wiki jana
walikuwa na kesi katika fisi ya chifu.
No comments
Post a Comment