NATO imesema Uturuki ina mashaka halali
Katika jitihada ya mataifa ya Finland na Sweden kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Jens Stoltenberg amesema Uturuki ina wasiwasi halali juu ya ugaidi na masuala mengine ambayo yanahitaji kupewa kwa uzito.
Wakizungumza katika mkutano wao wa pamoja rais wa Finland Sauli Niinisto, na Stoltenberg walisisitiza hakuna taifa jingine kwenye ushirikiano wa NATO ambalo limekabiliwa zaidi na mashambulizi ya kigaidi zaidi ya Uturuki.
Na hivyo kuyanyooshea vidole mataifa yake jirani yenye hali tete kama Iraq na Syria kuwa ni sehemu ya kadhia hiyo.Uturuki inayoyashutumu mataifa ya Finland na Sweden kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Kikurdi imesema haitaunga mkono mataifa hayo mawili kujiunga na NATO hadi wabadilishe sera zao.

No comments
Post a Comment