Umoja wa Mataifa yaitaka Iran kuanzisha mazungumzo ya nyuklia yaliokwama
Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia, IAEA, limeitaka Iran kuanzisha upya majadiliano kuhusu nguvu za Atomiki, ili kuepusha ugumu wa kufanikisha utelezwaji wa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015, Katika mkasa ulioripotiwa juma hili Iran ilizima baadhi ya kamera zilizokuwa zinawasaidia wakaguzi wa kimataifa kutimiza wajibu wao.
Katika mahojiano yake na kituo cvha televisheni cha CNN, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Rafael Grossi amesema kamera 27 zimeondolea katika vinu vya nyuklia, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni mbaya ambayo suluhu yake inapaswa kuwa mazungumzo ili utaratibu uendelee kama kawaida.
Makubaliano ya nyuklia wa 2015 ya mpango wa utekelezaji wa pamoja wa nyukilia unatoa unafuu wa kuondolewa vikwazo kwa Iran kwa ahadi ya kuachana na matumizi yake tata ya nyuklia.

No comments
Post a Comment