NMB yasaidia ukusanyaji wa trilioni 8.6 za Serikali
Benki ya NMB
kupitia mifumo yake mbali mbali ya malipo imesaidia Serikali kukusanya trilioni
8.6 kupitia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) kwa miaka
mitatu kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.
Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna
wakati wa warsha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa watendaji mbalimbali wa Mkoa
wa Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos
Makalla, Wakuu wa Wilaya, madiwani, watendaji na waweka hazina.
Zaipuna alisema benki yake imeendelea kuwekeza kwenye teknolojia jambo
ambalo limesaidia kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi huku
akisisitiza kuwa benki yake imejizatiti kuendelea kutoa bidhaa zinazokidhi
mahitaj ya wateja wake.
“Ubunifu ni kitu pekee ambacho kimetusaidia kupiga hatua na ule
uwekezaji ambao tuliufanya kwenye teknolojia ulituwezesha kuwa benki ya kwanza
kuunga mifumo yetu na Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) na
hadi sasa zaidi ya taasisi 1,100 tayari zimeunga mifumo yake kwenye mifumo ya
NMB ya ukusanyaji wa mapato,” alisema.
Zaipuna alisema ukusanyaji wa mapato kupitia mfumo wa kielektroniki
umekuwa ukongezeka kutoka 2.1 trilion mwaka 2019 hadi 3.7 trilioni mwaka jana.
“Fedha hizi zilikusanywa kupitia mifumo yetu ya NMB mkononi, NMB Wakala,
Lipa Namba, intaneti nk. Tunaendelea kuwekeza kuhakikisha kuwa mtandao wetu upo
vizuri na kuhakikisha usalama wa malipo,” Alisema.
Aidha, Zaipuna alisema benki yake imekuwa mstari wa mbele katika
kuchangia maendeleo ya jamii nchini kote nakuongeza kuwa benki yake kwa
makusudi ilizindua taasisi yake ya NMB Foundation ilikuchangia maendeleo
endelevu.
Alisema Benki yake kwa makusudi iliamua kutenga asilimia moja ya faida
yake kila mwaka kuchangia maendeleo nchini kote kwenye sekta za elimu, afya,
kilimo, mazingira, uwezeshaji na matukio ya dharura.
Zaipuna
alisema benki yake itaendelea kushirikana na wadau mbali mbali wa maendeleo
ikiwemo serikali ilikuleta maendeleo chanya na endelevu.
Naye Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla wakati wa warsha hiyo alishukuru benki
ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono jitihada mbali mbali za Serikali za kuleta
maendeleo kwa wananchi wake.
Makala alisema utendaji mzuri wa
benki hiyo umetokana na mazingira mazuri ya kibiashara ambayo yamewekwa na
serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan huku
akisisitiza kuwa Serikali itandedelea kuboresha mazingira ya kubiashara
ilikuvujia wawekezaji wengi nchini.
“Benki ya NMB imekuwa mstari wa
mbele kuchangia shughuli zetu za serikali. Serikali ina hisa kwenye benki hii
na juzi tu wametoa gawio kwa serikali. Tutaendelea kushirikiana na Benki ya NMB
ili kuboresha mazingira ya wananchi wetu,” alisema Makalla.
Makalla aliitaka benki hiyo kuendelea kubuni bidhaa mbali mbali zinazogusa wananchi kuanzia ngazi ya chini na kusisitiza kuwa Serikali itaendela kuchangia ushirikishwaji wa kifedha.
No comments
Post a Comment