Jafo na ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji
wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 22, 2022.
Akizungumza mara baada ya kukagua jengo hilo Dk. Jafo alionesha
kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo akimtaka mkandarasi Kampuni ya SUMA
JKT kuongeza kasi ya ujenzi ili likamilike na hatimaye lianze kutumika.
Dkt. Jafo
aliishukuru Kampuni ya SUMA JKT ambayo imepewa kazi ya kutekeleza mradi huo kwa
hatua iliyopiga pamoja na kamati iliyoteuliwa kuusimamia ujenzi huo.
“Pamoja na kuwa mradi huu
tunatakiwa tuukamilishe Novemba tisa mwakani ya miaka miwili lakini ikiwezekana
hata ukamilike haraka zaidi na, ijapokuwa mkataba unasema kazi inaisha mwaka
mmoja lakini ikiwezekana by mwanzoni mwa mwakani iwe imekamilka,” alisema Jafo.
Hata hivyo waziri huo alitoa
maelekezo kwa wakandarasi wote wanaojenga majengo ya Serikali katika maeneo
mbalimbali kuweka mfumo kuvunia maji ya mvua ili kunusuru athari za mafuriko
pamona kuwa na hifadhi ya maji.
Awali akiwasilisha taarifa ya
mradi huo Karani wa Mradi wa Ujenzi Bi. Philomena Bango alisema kazi mbalimbali
zinaendelea kutekelezwa kulingana na mpango kazi (master program) uliowekwa.
Bi. Philomena aliongeza kwa
kusema kuwa hadi kufikia sasa mkandarasi ameshakamilisha kazi ya ujenzi wa
mradi kwa asilimia 33 na kuwa wana matumaini ya utakamilika kwa wakati.
Hata hivyo, alisema kuwa
mkandarasi huyo anakabiliwa na changamoto ya kupanda kwa gharama za vifaa vya
ujenzi vikiwemo nondo.
Ofisi ya Makamu wa Rais ilisaini mkataba wa sh. bilioni
18.8 na Kampuni ya SUMA JKT wa kuanza ujenzi huo Oktoba 13, 2021 na kukabidhi
rasmi eneo la ujenzi kwa Mkandarasi baada ya kushinda zabuni ambapo ujenzi wake
unasimamiwa na Msimamizi Elekezi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
No comments
Post a Comment