Halmashauri ya Nzega yatakiwa kuwasilisha makato ya mifuko ya hifadhi ya jamii
Halmashauri ya
wilaya ya Nzega mkoni Tabora imetakiwa kuwasilisha Makato ya mishahara
kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii PSSSF ambayo hayakuwasilishwa kiasi
cha shilingi milioni 104,686,299 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt
Batilda Burian wakati wa Baraza maalumu la madiwani kujadili
taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa
fedha 2020/2021.
Alisema kwamba
licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi lakini fedha za watumishi zinapaswa
kuwasilishwa kwenye eneo husika ili kuepusha usumbufu na adhabu zisizo na
msingi.
“Katika hoja hii naelekeza
halmashauri kupeleka makato PSSSF kwa wakati ili kuepuka adhabu ya matumizi ya
Fedha yasiyokuwa na faida”alisema Balozi Dkt Batilda .
Alisema kwamba fedha za makato ya
wafanyakazi ni ni haki yao kuwasilishwa kwenye mifuko ya jamii ili iweze
kunufaisha watumishi hao mara baada ya kumaliza utumishi wao.
Katika hatua nyingne Mkuu
huyo wa mkoa wa Tabora amemtaka mkurungezi wa halmashauri ya wilaya ya
nzega Kiomoni Kibamba kuwachukulia hatua za kisheria vikundi
vitakavyokaidi kurejesha fedha walizokopa ikiwemo wakuwafikisha mahakamani.
Balozi Dkt Batilda
alisema kwamba Kutokurejeshwa kwa mikopo ya asilimia 10 iliyotolewa
kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ni kufifisha juhudi za
halmashauri na serikaliya mkoa .
Alisema kwamba fedha hizo ni
kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita kiasi cha shilingi milioni
145,133,500.00 kitu kinachorudisha nyuma jitiada za serikali kuhakikisha kundi
kubwa la watu wanapatiwa mikopo hiyo .
“Naomba nipewe mpango mkakati wa
jinsi fedha hizi zitarejeshwa ili waweze kukopeshwa makundi mengine kwani
uhitaji ni kubwa sana wa mikopo hiyo”alisema Balozi Dkt Batilda
Halmashauri ya wlaya ya Nzega
mkoani hapa kwa mwaka wa Fedha 2020/21, imepata hati safi imetokana
na kuzingatiwa kwa viwango vya Uhasibu vya Kimataifa vya uandaaji wa
taarifa za Fedha katika Taasisi za Umma (IPSAS).
No comments
Post a Comment