Jeshi la uhamiaji limetenga siku 10 kusaka wahamiaji haramu Loliondo
Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ametangaza kuanza kwa operesheni maalum
ya siku kumi kusaka wahamiaji haramu katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani
Arusha.
Kamishna Jenerali
Makakala amebainisha hayo leo Loliondo, na kusema kuwa zoezi hilo litaenda
sawia na zoezi linaloendelea la uwekaji wa alama za mipaka katika Pori Tengefu
la Loliondo.
Dkt. Makakala
amesisitiza kufuatwa kwa sheria za nchi pale wageni wanapotaka kuingia au
kutoka nchini, na kwamba Uhamiaji imejipanga vema kusimamia eneo hilo katika
mipaka yote nchini.
“Nchi yetu
imebarikiwa kwa kuwa na maeneo mazuri ambayo yanavutia wahamiaji haramu kufika
nchini kwa sababu tofauti, hatutakubali hilo litokee wakati wowote ule,”
alisema Makakala.
Kwa upande wake,
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mwalimu Raymond Mangwala amemfahamisha
Dkt.Makakala kuwa wilaya yake inaendelea vema na utekelezaji wa zoezi la
uwekaji wa alama za mipaka katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo na kwamba
atatoa ushirikiano katika zoezi la kusaka wahamiaji haramu ili wale wote
watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi.
No comments
Post a Comment