Header Ads

Header ADS

Ajali ya Treni Tabora yaua watu wanne

 


Mabehewa sita ya Treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea Mkoani Tabora  mpaka Dar es salaam, yameanguka katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, ACP. Richard Abwao amesema kuhusu majeruhi na vifo bado jeshi linaendelea  kufuatilia kutokana na  abiria wengi kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete, kwa ajili ya matibabu.

Aidha amesema chanzo cha ajili hiyo mpaka Sasa bado hakijulikani na ufuatiliaji bado unaendelea.

Awali Shirika la Reli Tanzania -TRC lilitoa taarifa ya ajali ya Treni ya Abiria namba Y14 yenye Injini namba 9019,iliyokuwa ikisafiri kutoka Kigoma kulekea Dar es salaam na kusababisha jumla ya vifo 4 na majeruhi 132 



No comments

Powered by Blogger.