Sanga awapongeza RUWASA Songwe kwa kukwamua miradi chechefu
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony
Sanga amewapongeza watendaji wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira
Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Songwe kwa jitihada zao za kuwafikishia wananchi
huduma ya maji.
Mhandisi Sanga ametoa pongezi hizo hivi
karibuni wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na RUWASA mkoani
humo.
“Nimejionea kazi kubwa na nzuri
inayofanywa na watendaji wetu wa RUWASA; Meneja wa RUWASA Mkoa wa Songwe na
Mameneja wako wa Wilaya mnafanya kazi nzuri,” alisema Mhandisi Sanga.
Alisema RUWASA ilipokea miradi mingi ambayo
ilikuwa haitoa maji ambapo kwa Tanzania nzima ilikuwa takriban miradi 177 na
kwamba kati ya hiyo miradi karibu 30 ilikuwa kwenye Mkoa wa Songwe na sasa
imekamilika isipokuwa mmoja ambao nao unatarajiwa kuanza kutoa maji hivi
karibuni.
“Kama ambavyo tumekuwa tukiongea miaka ya
nyuma tulikuwa na miradi mingi sana ambayo tunaita miradi chechefu takriban
miradi 177 na katika mkoa huu peke yake kulikuwa na miradi chechefu karibu 30
na tunafurahi kuona miradi takriban yote imekwamuliwa katika mkoa huu wa Songwe
umebaki mmoja tu nao unakaribia kukamilika,” alifafanua Mhandisi Sanga.
Alisema ukamilishwaji wa miradi hiyo ni
faraja kwa Serikali kwani inakuwa imetimiza dhamira na ahadi yake ya kumtua
mwanamke ndoo kichwani na aliwasisitiza kuendelea na jitihada za kuwaondolea
adha wananchi.
Mhandisi Sanga alisema matarajio ya Serikali
ni kuhakikisha vyanzo toshelevu vya maji vinatumika kote nchini ili kuwaondolea
adha wananchi na kwamba ziara yake mkoani humo ni hatua mojawapo ya kutazama ni
vipi suala hilo linafanikiwa.
Naye Diwani wa Kata ya Uwanjani Wilaya ya
Tunduma, Kwintin Kayombo akizungumza kwa niaba ya wananchi wake alipongeza
jitihada za Wizara ya Maji kwa harakati zote inazoendelea nazo katika
kuhakikisha wanapata huduma ya majisafi na salama.
“Kwa niaba ya wananchi hawa tumepata faraja kubwa sana baada ya kuona mradi huu wa tenki kwenye kata yetu ambao utahudumia pia na kata zingine tatu kwenye wilaya yetu; tunashuhudia mambo makubwa yakifanywa na Wizara ya Maji,” alisem
Mradi wa ujenzi wa tenki la maji litakalohudumia Kata za Uwanjani, Mwakakati, Majengo mapya na Msasani
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga (kulia) watendaji Wizara ya Maji wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Uwanjani, Kwintin Kayombo (kushoto) walipotembelea mradi wa ujenzi wa tenki kwenye kata hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga (mwenye kofia ngumu) akikagua ujenzi wa tenki la maji Kata ya Uwanjani Wilayani unduma.
No comments
Post a Comment