Sillo Mbunge wa Kwanza Manyara kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani 2020-2021
Taarifa hiyo ya utekelezaji wa ilani iliyochapishwa katika kitabu chenye kurasa 47, imekuwa na mvuto wa kipekee kwa kuwa imeelezea jiografia nzima ya halmashauri ya jimbo la Babati vijijini, shughuli za kiuchumi ndani ya jimbo.
Sillo ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo wa kuchaguliwa, kwa awamu ya kwanza, amedhihirisha sifa yake hiyo, baada ya kuwasilisha Taarifa ya Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi hicho katika Mkutano wa wajumbe wa Halmashauri uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliopo Mjini Babati.
Aidha taarifa hiyo imeainisha vipaumbele vya kimaendeleo pamoja na miradi ya kimkakati pamoja na fedha za mfuko wa jimbo zilizopokelewa kwa mwaka 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 70,170,000 ambazo ziligawanywa katika kata zote 25 za jimbo hilo kulingana na maombi yaliyotumwa kwenye ofisi ya mbunge.
No comments
Post a Comment