Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Moscow kwa "kichaa" baada ya wanajeshi wa Urusi kushambulia kiwanda cha kemikali katika harakati zao za kukamilisha kuuteka mji muhimu wa mashariki.

Vikosi vya Urusi vilishambulia tanki la asidi ya nitriki huko Severodonetsk, na kumfanya gavana wa eneo hilo kuwaonya watu kusalia ndani ya nyumba.

Katika hotuba yake ya usiku kucha, Zelensky alisema: "Kwa kuzingatia uwepo wa uzalishaji mkubwa wa kemikali huko Severodonetsk, shambulizi la jeshi la Urusi huko, pamoja na ulipuaji wa mabomu ya anga, ni wazimu tu."

Vita vya Severodonetsk vimekuwa vikali zaidi katika siku za hivi karibuni, na majeruhi makubwa katika pande zote za Ukraine na Urusi.