Marekani itaitumia Ukraine mifumo ya juu zaidi ya roketi kuisaidia kujilinda, Rais Biden ametangaza.

Silaha hizo, zilizoombwa kwa muda mrefu na Ukraine, ni kusaidia kushambulia vikosi vya adui kwa usahihi kutoka umbali mrefu.

Hadi sasa, Marekani ilikuwa imekataa ombi hilo kwa kuhofia silaha hizo zinaweza kutumika dhidi ya shabaha nchini Urusi.

Lakini siku ya Jumatano, Bw Biden alisema msaada huo utaimarisha msimamo wa Kyiv wa mazungumzo dhidi ya Urusi na kuleta suluhu la kidiplomasia zaidi.

Akiandika katika gazeti la New York Times, alisema: "Ndiyo maana nimeamua kuwa tutawapa Waukraine mifumo ya juu zaidi ya roketi na zana ambazo zitawawezesha kushambulia kwa usahihi shabaha muhimu kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine."

Silaha mpya zitajumuisha Mfumo wa Roketi wa Kivita wa M142 (HIMARS), afisa mkuu wa Ikulu ya White House alisema - ingawa hakufafanua ni ngapi kati yao zitatolewa.

Mifumo hiyo inaweza kurusha makombora mengi ya kuongozwa kwa usahihi katika shabaha hadi kilomita 70 (maili 45) - mbali zaidi kuliko mizinga ambayo Ukraine inayo sasa hivi. Pia inaaminika kuwa sahihi zaidi kuliko silaha za Urusi