Rais wa Angola João Lourenço wa Angola anasema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekubali kuwaachilia wanajeshi wawili wa Rwanda iliyowashikilia wiki jana, huku kukiwa na mvutano unaoongezeka wa mpaka.

Bw Lourenço - ambaye anahudumu kama mpatanishi - alitoa tangazo hilo baada ya mazungumzo tofauti na wenzake wa Kongo na Rwanda.

Ofisi yake ilisema Félix Tshisekedi na Paul Kagame walikubaliana kukutana ana kwa ana nchini Angola, lakini haikutoa tarehe.

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeshutumu kila mmoja kwa kusaidia wanamgambo wenye silaha katika eneo la mpaka na kuhimiza mashambulizi.

Wakongo wafanya maandamano ya kuipinga Rwanda

Kwingineko Mamia ya watu waliingia katika mitaa ya mji mkuu wa Kongo, Kinshasa, kulaani madai ya Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23.

Maandamano hayo yaliandaliwa na shirika la kiraia, NDSCI.

Siku ya Jumatatu, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais wa Senegal Macky Sall, aliwapigia simu viongozi wa Rwanda na Kongo kujaribu kupunguza mvutano kati ya Kigali na Kinshasa.

Pande zote mbili zinashutumu kila mmoja kwa kuunga mkono makundi ya waasi mashariki mwa DR Congo.

Bwana Sall hapo awali alielezea "wasiwasi mkubwa" kutokana na kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili.