Utalii wa ndani: Wanafuzi chuo cha GITC Makambako wafanya ziara hifadhi ya Mikumi
Katika jitihada za kuunga mkono kampeni ya Royal Tour
iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa
habari na utalii Grossal Institute Training College kilichopo Makambako mkoani
Njombe,kimefanya utalii wa ndani kwa kutembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi.
Akizungumzia ziara hiyo mkuu wa chuo cha GITC, Bwana George Mwita amesema lengo kubwa la kufanya ziara hiyo ni kwamba wanafunzi wajifunze kwa vitendo yale wanayoyasoma darasani, pia ni
Mwita ameongeza kuwa chuo kilichagua kutembelea hifadhi hiyo
kutokana na ukubwa wa hifadhi hiyo
“Sisi tumechagua kutembelea hifadhi hiyo ni kutokana na
uwepo wa vivutio vingi ndani ya hifadhi hiyo, hafu ni moja kati ya hifadhi
kubwa kwa hapa nchini, sio kwamba hifadhi zingine hazina vivutio ila sisi
tuliamua kwenda huko”
Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho walisema ziara hiyo
imewaongezea uelewa kuhusu vitu walivyokuwa wanavisoma darasani, huku wakisisitiza
jamii kuwa na tabia ya kutembelea vivutio vinavyopatikana ndani ya nchi yetu.
Hifadhi ya Mikumi ni ya saba kwa ukubwa miongoni mwa hifadhi
zinazopatikana Tanzania, na ina ukubwa wa km 1930.
Huu ni muendelezo wa ziara mbalimbali zinazofanywa na wanafuzi wa chuo cha GITC Makambako, katika jifunza kwa vitendo.
No comments
Post a Comment