Watu 6 wauawa katika mashambulizi
Mashambulizi ya kuwalenga watu wengi huko Philadelphia, Pennsylvania, na Chattanooga katika jimbo la Tennessee, yameua watu sita na kujeruhi wengine zaidi ya 25, polisi wamesema Jumapili.
Washambuliaji wengi walifyatua risasi kwenye barabara ya Philadelphia ya South Street yenye shughuli nyingi, eneo lenye baa nyingi na migahawa, nyakati za saa sita usiku Jumamosi. Wanaume wawili na mwanamke mmoja waliuawa, maafisa wamesema.

“Kulikuwa na mamia ya watu wakifurahi kwenye barabara ya South Street, kama wanavyofanya kila mwishoni mwa juma, wakati ufyatuaji wa risasi ulipoanza,” mkuu wa polisi huko Philadelphia D.F. Pace amesema.
Katika tukio jingine, watu watatu waliuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya shambulio la risasi karibu na baa moja katika mji wa Chattanooga, maafisa wamesema, wakiongeza kuwa watu wawili walifariki kutokana na majeraha ya risasi na mmoja alifariki kufuatia majeraha baada ya kugongwa na gari akikimbia kutoka kwenye eneo la tukio.
Waathirika watatu walijeruhiwa wakati wakijaribu kukimbia na waligongwa na magari, maafisa wa Tennessee wamesema, wakiongeza kuwa wengine kadhaa waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.
Hapa Marekani mwaka huu, kumefanyika mashambulizi 240 yanayolenga watu wengi.
No comments
Post a Comment