Wananchi kuhamasishana kuongeza juhudi kuzaa kisa Zahanati
Wakazi wa kijiji cha Ivilikinge wilaya ya Makete mkoani Njombe,wameanza kuhamasishana kushika mimba na kuzaa kutokana na kujengwa Zahanati kubwa ukilinganisha na iliyokuwepo awali yenye miundombinu chakavu na huduma za matibabu zilizokuwa sio za uhakika.
Wameanza
kubainisha hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda wakati
akipokea msaada wa mabati 200 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika kijiji
hicho ambao umetolewa na benki ya NMB.
Wakizungumza baadhi
ya wakazi wa kijiji hicho wamesema jingo la awali la zahanati hiyo ni dogo
ambalo lilikuwa likipelekea kuwepo kwa mrundikano wa wagonjwa wengi hadi
wengine kukosa sehemu ya kupumzishwa baada ya kupata matibabu na kusababisha
wanawake kijijini hapo kusitisha kushika mimba na kuzaa watoto kutokana na hofu
ya kupoteza maisha.
"Kuanzia
sasa sisi wanawake tuhamasishane kuzaa kwa kuwa jengo hili la zahanati
inayojengwa sasa itakidhi mahitaji na tutajifungua salama" alisema mmoja
wa wakazi hao
Mkuu wa wilaya
hiyo Juma Sweda mara baada ya kupokea msaada huo wa mabati ambayo thamani
yake ni 8.5 milioni alisema utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa
zahanati utafanyika haraka iwezekanavyo ili wananchi wa kijiji hicho waweze
kunufaika na huduma za afya.
"Kwakuwa
zahanati hii itaisha niwaombe NMB mtuongezee vitanda na tukishafanya hivyo
wakina mama wapo wanataka kujifungua na wapo tayari kushika mimba na
serikali ya mama Samia inasema kushika mimba na kijifungua ni bure"
alisema Sweda.
No comments
Post a Comment