Watuhumiwa wa mauaji Kiteto wafikishwa Mahakamani
Watu 16 wanatuhumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja aliyefahamikwa
kwa jina la Enj Angel Mwaisumwa(34) mkazi wa Kata ya Matuo wilayani Kiteto
mkoani Manyara.
Tukio hilo lilitokea June 10
mwaka 2022 Kijiji cha Engusero Wilayani Kiteto Mkoani Manyara baada ya
kutuhumiwa kukutwa na viungo vya binadamu maarufu kama vocha.
Waliofikishwa mahakamani na
kusomewa shitaka la mauaji kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 ni, Ngalawa Msafiri, Bilali Mohamed, Salimu
Halouna, Rajabu Mbarouk, Paulo Jackson, Zulfa Issa, Emmanuel Pallangya na Salimu
Rashid
Wengine ni Jonas Harod, Malaki
Julius, Salmini Adamu, Ramadhani Husein, Chales Ngole, Athumani Hamad,
Ramadhani Amir na Isaya Emmanuel
Akisoma mashitaka hayo mwendesha
mashtaka wa Jeshi la Polisi Kiteto, Joseph James Soke mbele ya hakimu mkazi wa
mahakama hiyo, Boniphas Lihamwike alimweleza hakimu huyo kuwa washtakiwa hao
walitenda Kosa kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2019
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja
walimsababishia kifo Anjel Allon 34, kuwa june 10 mwaka 2022, katika Kijiji cha
Engusero Kata ya Engusero kuwa walimpiga hadi kufa mwanamke huyo wakimtuhumu
kuwa na viungo vya binadamu
Washitakiwa hao hawakutakiwa
kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi
hiyo
Kesi hiyo imekuja kwa kutajwa
mahamamani hapo na baada ya siku 14 itakuja tena kwa kutajwa
No comments
Post a Comment