Header Ads

Header ADS

Wapiganaji watatu wa Marekani waripotiwa kutoweka Ukraine

 Wapiganaji watatu wa Marekani waripotiwa kutoweka UkraineWizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema inafahamu kuhusu ripoti kwamba wapiganaji watatu wa Kimarekani wametoweka nchini Ukraine, huku wawili kati yao wakihofiwa kukamatwa.

Maveterani wawili wa kijeshi waliokuwa wakipigania Ukraine walitajwa katika ripoti za wiki hii kuwa walichukuliwa mateka.Idara ya serikali ilisema Alhamisi: "Kuna ripoti za Mmarekani mmoja wa ziada ambaye hajulikani aliko.

"Wiki iliyopita, wafungwa watatu wa kigeni walihukumiwa kifo kwa kuisaidia Ukraine.Wanaume hao wawili wa Uingereza na mwanamume mmoja wa

Morocco walihukumiwa na mahakama ya kujitenga inayoungwa mkono na Urusi huko Donetsk kunyongwa kwa kupigwa risasi na askari.

Ikulu ya White House ilisema Alhamisi "inafanya bidii sana kujifunza zaidi" kuhusu ripoti ambazo hazijathibitishwa za Wamarekani waliopotea au waliotekwa nchini Ukraine.

Kundi la wanajeshi wa zamani wa Marekani na Ufaransa walituma ujumbe katika tweeter Jumatano kwamba Wamarekani wawili waliokuwa nao walikamatwa wiki moja iliyopita.

Iwapo ripoti hiyo itathibitishwa, hawa watakuwa Wamarekani wa kwanza kupigania Ukraine kutekwa tangu vita kuanza mwezi Februari.





No comments

Powered by Blogger.