Augustine Okrah sasa ni nyekundu na nyeupe
Klabu ya Simba SC imetambulisha Rasmi Kiungo
Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Augustine Okrah, kwa Mashabiki na Wanachama wa
Klabu hiyo ya Msimbazi.
Simba SC imemtambulisha mchezaji huyo kupitia
Simba APP na Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, leo Jumatano (Julai 13), saa
saba mchana.
Okra amesajiliwa Simba SC akitokea Bechem
United ya nchini kwao Ghana, kwa mkataba wa miaka miwili.
Inadaiwa Kiungo huyo amekamilisha usajili wake
Msimbazi kwa dau la dola za Kimarekani 120,000 ambazo ni zaidi Shilingi Milioni
280 za Kitanzania.
Msimu uliopita Okrah mwenye umri wa miaka 28
alifunga mabao 18 (Ligi Kuu ya Ghana 14 na Kombe la FA 4), huku akitoa pasi
saidizi (assist) 10 (Ligi Kuu 6 na Kombe la FA 4), akiwa na kikosi Cha Benchem
United.
Kabla ya kutua ya kutua Simba SC, Okrah amewahi
kuitumikia Asante Kotoko, RB Ghana FC na North East FC (zote za Ghana), Al
Merreikh na Al Hilal (Sudan), Hacken (Senegal) na Smouha FC (Misri).
No comments
Post a Comment