Rais ateua mrithi wake, akimbia nchi
Waziri Mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe
ambaye naye alitangaza kujiuzulu hii leo ameteuliwa kuwa Rais wa
mpito wa nchi hiyo.
Spika wa Bunge la Sri Lanka, Mahinda Yapa
Abeywardena amesema Waziri Mkuu ameteuliwa kuwa Kaimu Rais baada ya Rais wa
nchi hiyo Gotabaya Rajapaksa kudaiwa kuikimbia nchi hiyo yeye na familia yake.
Hata hivyo Spika huyo amesema uteuzi wa Waziri
Mkuu kukaimu nafasi hiyo umefanywa na Rais Gotabaya Rajapaksa kabla hajaondoka
nchini humo.
“Alinifahamisha
kuhusu uteuzi huo chini ya Kifungu cha 37.1 cha katiba ya nchi yetu ya Sri
Lanka,” amesema Spika Mahinda Yapa.
Hatahivyo, hakuna neno la moja kwa moja
lililotolewa na Rais Rajapaksa mwenyewe, ingawa matangazo yote ya nchi katika
siku zote za hivi karibuni katika siku za hivi karibuni yametolewa na Spika wa
Bunge na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa Katiba ya Sri Lanka, nafasi ya
Rais ikiwa wazi, Waziri Mkuu ataapishwa na kukaimu kwa muda mpaka
atakapochaguliwa Rais mwingine kutoka miongoni mwa wabunge.
Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ameikimbia
nchi hiyo kwa ndege ya kijeshi, huku kukiwa na maandamano makubwa kuhusu mzozo
wa kiuchumi.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 amekimbilia Maldives.
Waziri Mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe ambaye ameteuliwa kukaimu nafasi ya Rais wa nchi hiyo.
No comments
Post a Comment