Rais akimbia nchi, wananchi washerekea
Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa
ameikimbia nchi kwa kutumia ndege ya jeshi kabla ya siku rasmi ya kujiuzulu
ambayo ni leo jumatano july 13, 2022.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka vyomba vya Habari
vya Kimataifa, zimesema kuwa Rais Gotabaya Rajapaksa amewasili nchini Maldives.
Rais Rajapaksa mwenye umri wa miaka 73,
alitarajiwa kukabidhi madaraka baada ya yeye na Waziri mkuu Ranil
Wickremesinghe kukubali kuachia ngazi.
Kujing’atua kwa mwanasiasa huyo, kunatamatisha
utawala wa ukoo wake ulioiongoza Sri Lanka kwa miongo kadhaa.
Wananchi wa Sri Lanka, wamesherehekea baada ya
kupata habari juu ya kukimbia kwa rais wao, Rajapaksa ambaye analaumiwa kwa
kusababisha mgogoro mkubwa wa kiuchumi.
Taarifa za kukimbia kwa Rais Rajapaksa akiwa na
mkewe na walinzi wake, zimetolewa na Shirika la habari la A
No comments
Post a Comment