CCM Tarime Waonya Wagombea Kupiga Kampeni Kabla Ya Mda Wake
Chama cha mapinduzi wilaya Tarime mkoani Mara
kimewatahatarisha wagombea waliochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani
ya chama hicho kusubiri mda wa kampeni ulifika na ikibainika wanapiga kampeni
watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya
Tarime,Valentina Daogratius Maganga a
kiongea na waandishi wa habari ofisini kwake alisema kuna wagombea taklibani 50
wamejitokeza kuchukua kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama
ikiwemo jumuia ya wazazi.
Katibu huyo alibainisha wagombea
waliochukua fomu kufikia sasa kuwa ni 50 kati yao wanawake waliochukua fomu za
kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama ni 11 huku walemavu ni mmoja na kuwa
mchakato huo ulianza julai 2 hadi kukamilika julai 10 jionp.
Maganga aliwataka kundi la wanawake
kujitokeza kwa wingi kuchangamkia frusa hiyo kwa kuwa kundi hili wanapewa
kipaumbele mfano wanaviti 4 kwenye halmashauri kuu ya wilaya.
Katibu huyo alitaja nafasi
zinazogombewa kuwa ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti wa CCM Wilaya nafasi moja
katibu siasa na uwenezi nafasi moja wajumbe wa halmashauri ya wilaya nafasi 10
wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa nafasi 2 wajumbe wa mkutano mkuu Taifa nafasi
3.
No comments
Post a Comment