Header Ads

Header ADS

Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA ] Chafanya kongamano la Katiba Mpya Mkoani Njombe

 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Njombe chini ya mwenyekiti wake Rose John Mayemba kimefanya kongamano lake mjini Makambako kwa ajili ya kuchochea vuguvugu la kudai katiba mpya ili nchi kuwa na kinachoelezwa kwamba ni ustawi na utengamano wa kitaifa na kuwa na dira ya maendeleo endelevu na kuheshimu haki za watu.

Pia Chama hicho kupitia kwa Katibu Mkuu Jonh Mnyika kimeitaka Serikali kutenga fedha kwaajili ya kukamilisha kwa wakati mchakato wa Katiba Mpya
Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Mnyika amewataka viongozi na wanachama wa Chama hicho kuendelea kupigania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ili kuzidi kujijenga chama hicho na kwenda kushinda kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Pia Askofu mkuu wa kanisa la Moravian la uamsho Tanzania na Afrika mashariki Mch.Emmaus Mwamakula ameshiriki kongamano la katiba mpya lililoandaliwa na CHADEMA mkoa wa Njombe mjini Makambako na kuwataka viongozi wa dini wenzake kuwa vielelezo katika kudai katiba mpya kwa madai kuwa katiba bora ni hitaji la watanzania kwa maendeleo endelevu ya taifa ili kujenga haki na ustawi wa Taifa na wananchi wake.






No comments

Powered by Blogger.