Header Ads

Header ADS

Chadema Tarime wawasha moto vuguvugu la katiba mpya.

 Kaimu mwenyekiti Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)kanda ya Serengeti,Gimbi Masaba alisema ajenda kuu ya chama chake ni kudai katiba mpya.

Masaba alisema hayo jana kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema jimbo la Tarime mjini ulioandaliwa na viongozi wake akiwemo katibu mwenezi,Pamba Chacha uliokalia ukumbi wa hoteli ya Blusky ili kujadili uhai wa chama pamoja na shuguli za maendeleo zilizofanyika kuanzia mwezi januari mwaka huu na miaka ya nyuma toka uchaguzi wa 2020.

“Ndugu zangu ajenda kuu ya chama chetu ni katiba mpya,suluhisho kwa usitawi na maendeleo kwa wananchi,viongozi na wafanyakazi kwa Taifa hili”alisema Masaba.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa kuna haja serikali kutoa ajira za mda mfupi kwa vijana kwa kutumia vigezo na wala sio kutumia njia ya mitandao jambo ambalo linawakwaza baadhi ya waombaji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema mkoa Mara,Lucas Ngoto alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kufanya kazi halali ya kujipatia kipato na kuondokana na swala zima la kutumiwa na wanasiasa kama  chambo.

Ngoto aliongeza kuwa zoezi la Sensa ni lakitaifa na lisifanyike kisiasa badala yake jamii na watu wote washiriki bila kujali itikadi ya vyama vinginevyo likifanyika kisiasa serikali iingilie kati

Naye mwenyekiti jimbo la Tarime mjini CHADEMA,Bashiri Abdallah (maarufu Sauti) alisema chama chake kimewachukulia baadhi ya wanachama wake pamoja na viongozi mbalimbali hatua ikiwemo kuwasimamisha uwanachama.

Mwenyekiti huyoaliwataka wanchama na viongozi kuwa na nidhamu kila moja kujali mwenzake kwa nafasi aliyonayo kwani kufanya hivyo chama kitasonga mbele na Taifa kwa ujumla.


Mwenezi jimbo la Tarime mjini,Pamba Chacha alisema kubadilishwa kwa viongozi mara kwa mara mfano wakuu wa wilaya mikoa na makatibu wake  kunatokana na katiba iliyopo na kuwa suluhisho ni katiba mpya.


No comments

Powered by Blogger.