Naibu waziri wa Sanaa ,Utamaduni na Michezo asisitiza watanzania kutenga Muda wa kufanya mazoezi
Mheshimiwa , Pauline Gekul amesema siri ya maisha ya afya njema ni kujitengea muda wa kufanya mazoezi ili kuwa salama kiafya na kuepuka magongwa yasiyoambukiza,.
Gekul, ameyasema hayo akiwa katika mjini Bagamoyo Mkoani Pwani, wakati akifunga mashindano ya mbio alizoshiriki za ‘Bagamoyo Marathon’ kwa kuhusisha wanariadha wa mbio za kilometa 21, kilometa 10 na na kilimeta 5.
“Watanzania tutenge muda wa kufanya mazoezi, nawahimiza wananchi wote tuendelee kufanya mazoezi katika maeneo yenu, maafisa michezo kote nchini msimamie vikundi vya jogging kwa kuhamasisha kupitia nyimbo za kizalendo ili kuwavuta watu wengi kushiriki kufanya mazoezi.
Hata hivyo, Gekul pia amezipongeza familia zilizojitokeza kushiriki mbio hizo na kusema ni muhimu kutengea muda wa mazoezi na wanafamilia kwa lengo la kuimarisha afya na kuepuka malazi nyemelezi yanayoepukika
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul akimvalisha medali mshindi kwanza kwa wanawake, Magdalena Shauri kutoka Jeshi la Wananchi (JWTZ), kutoka Arusha.
Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya For Better Life, Dkt. Deogratius Soka amesema mbio hizo ni hamasa katika mchezo wa riadha nchini, kuongeza ajira kwa vijana, kukuza utalii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi.
No comments
Post a Comment