DRC yawa mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo sasa ni mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC).
DRC imeidhinishwa rasmi kuwa mwanachama wa saba wa
EAC baada ya Christophe Lutundula, Naibu Waziri Mkuu Anayeshughulikia Masuala
ya Nje ya Kongo DR kukabidhi nyaraka kwa makao makuu ya jumuiya hiyo ya kikanda
huko Arusha, Tanzania.
Hatua ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
kuidhinishwa rasmi kuwa mwanachama kamili wa EAC ina maanisha kuwa, nchi hiyo
sasa ina haki zote za nchi mwanachama wa jumuiya hiyo, na itafaidi mambo mengi
kama wanachama wengine.
Baadhi ya mambo itakayofaidi DRC baada ya
kupasishwa rasmi kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni
kuruhusiwa raia wake kuingia katika nchi wanachama wa jumuiya bila viza.
Vile vile soko lake litapanuka kutokana na
uagizaji na usafirishaji huru wa bidhaa hususan katika maeneo ya mashariki ya kanda
hiyo ya Afrika, yanayotegemea bandari za Mombasa na Dar es Salaam. Aidha nchi
hiyo sasa ina haki ya kuteua wanachama 9 wa Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EALA) na majaji wa Mahakama ya Uadilifu ya jumuiya hiyo EACJ.
Peter Mathuki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki amesema mchakato wa DRC kujiunga na jumuiya hiyo umekamilika, na sasa
ni rasmi nchi hiyo ni mwanachama kamili wa EAC.
Sudan Kusini ilikuwa nchi ya mwisho kukubaliwa
kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi Machi mwaka 2016, kabla ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kukubaliwa kujiunga na jumuiya hiyo Machi
mwaka huu.
No comments
Post a Comment