Anayedaiwa kumuua house girl wake kisha kuficha mwili kwenye stoo ya vifaa vya ujenzi akamatwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata Selemani Haruna maarufu Kwata (24), kwa tuhuma za kumuua Editha Charles (22), Binti wa kazi za ndani na kuuficha mwili huo katika stoo ya vifaa vya ujenzi katika nyumba ya Agatha Stanslaus Jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa uchunguzi wa awali umeonesha mnamo Julai
06, 2022 majira ya asubuhi mtuhumiwa huyo alifika kwenye nyumba aliyokuwa
anayoishi Binti huyo wa kazi akijifanya fundi wa umeme na kwamba alitakiwa
kuweka Balbu.
Kamanda Muliro amesema kuwa baada ya
kuingia alimshambulia kwa kitu chenye ncha kali Binti huyo na kumuua halafu
akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba Tsh 1,800,000 na kutoweka.
“Polisi kwa Kutumia Watalaamu wake wa
uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi walibaini Mtuhumiwa
huyo kuwa aliingia kwenye nyumba hiyo na kukaa kwa masaa kadhaa na kutoka"
amesema Kamanda Muliro
Ameongeza kuwa baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina alikiri kumuua Binti huyo, kuvunja mlango wa chumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000 na mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane.
Kamanda Muliro amesema kitendo
alichofanya Mtuhumiwa ni cha ukatili uliopitiliza na kuongeza baada ya
Uchunguzi kukamilika atafikishwa Mahakamani.
No comments
Post a Comment