Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa
Jinai (DCI), mshukiwa alimuua Josephat Kibet mwenye umri wa miaka 31 kufuatia
mzozo wa kuchaji simu.
Taarifa ya DCI inasema kuwa mzozo kati
ya wawili hao ulizuka jioni ya Jumapili, Julai 10, na kinda huyo kumshambulia
binamu yake.
“Polisi eneo la Kaimosi, Kaunti ya
Nandi wanamtafuta mshukiwa wa miaka 17 ambaye alimuua binamu yake jioni ya
Jumapili kufuatia mzozo wa kuchaji simu. Kufikia sasa uchunguzi unaonyesha kuwa
wawili hao walikuwa wakizozana kuhusu ni nani wa kuchaji simu yake wa kwanza,”
DCI ilisema kupitia kwa taarifa.
Mshukiwa anaripotiwa kuchomoa mshale na
kumdunga binamu yake kabla ya kukimbilia mafichoni.
“Mvulana huyo alikimbia mshale na
kumdunga mwendazake upande wa kushoto wa kifua kabla ya kutoroka,” DCI ilisema.
Josphat KIbet alikimbiza katika
Hospitali ya Rufaa ya Kapsabet lakini akawa ameaga dunia hata kabla ya
kufikishwa hospitalini.
“Josphat Kibet alithibitishwa kuaga
dunia alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kapsabet kufuatia majeraha na
mshale kutoka kwa kinda huyo,” taarifa ya DCI inasema.
No comments
Post a Comment