Kesi ya akina Mdee kutolewa yuamuzi Julai 6
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa
maombi ya Mbunge wa viti maalum wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
Halima Mdee na wenzake 18 kuomba kibali cha mahakama kufanya mapitio ya
kimahakama kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.
Halima Mdee na wenzake wamewasilisha
ombi hilo wakiwa na hoja tano za kisheria ikiwemo, kufungua maombi hayo ndani
ya muda wa kisheria na kuonesha maslahi yao mapana kwa Chadema na kama Wabunge
wametafuta haki zao ndani ya chama hicho hadi ngazi ya juu.
Akiwasilisha hoja hizo, mmoja wa
mawakili wa wabunge hao Ipilinga Panya amedai waliopeleka kuwa waliopeleka maombi
wote kumi na sita wanamaslahi katika jambo hilo kwani wamekuwa waathirika wa
maamuzi ya Bodi ya Wadhamini ya chama hicho kupitia uamuzi wa Baraza kuu la
CHADEMA lililofanyika Mei11 mwaka huu na kufukuzwa uanachama.
Pia amedai kuwa waliopeleka maombi
wote ni Wabunge wa viti maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
walioteuliwa na Bodi ya Chama hicho mwaka 2020/2025 hivyo maamuzi ya kuwafukuza
uanachama bila kufuata utaratibu wa kuwasikiliza kunagusa maslahi yao binafsi
kama wanachama wa chama cha siasa na wabunge wa Bunge la Tanzania.
Wakili mwingine wa wabunge hao Ebson
Kilatu amedai kitendo cha baraza hilo kuwafukuza uanachama hawakuzingatia haki
wakati wa utoaji maamuzi hayo.
Akijibu hoja hizo kwa niaba ya Baraza
la Wadhamini la CHADEMA Wakili Peter Kibatala amedai hawapingi hoja ya wabunge
hao kuwa na maslahi mapana ila kigezo cha mgogoro huo kuwepo Ushahidi
mahakamani ili ichunguze huo Ushahidi wao na mahakama ijiridhishe na kutoa
uamuzi.
Amedai mahakama hiyo haiwezi kuwapa
nafuu ianazoomba walioleta maombi kwa sababu wamewasilisha maombi hayo nje ya
muda.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Julai 6
mwaka huu itakapotolewa uamuzi.
No comments
Post a Comment