Wananchi Singida watahadharishwa kutouza chakula ovyo
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge, amewatahadharisha wananchi kutouza
chakula ovyo walichonacho kwani hali sio nzuri kutokana na maeneo mengi
kutopata mvua za kutosha msimu huu na hivyo kupata mavuno kidogo ambayo kama
wakiyauza bila mpangilio wataweza kukumbwa na balaa la njaa.
Ametoa
tahadhari hiyo wakati akizungumza na wananchi mjini Ikungi ikiwa ni mfululizo
wa ziara zake za kusikiliza kero mbalimbali za wananchi katika wilaya zote za
mkoa huu na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.
Hatua
ya Mkuu wa Mkoa kutoa tahadhari hiyo ilifuatia ombi la wananchi wa Kata ya
Ikungi kutoa ombi kwa serikali iwapatie chakula cha msaada ambacho kitauzwa kwa
bei nafuu kwa kuwa msimu huu wa kilimo hali ya chakula ni mbaya kwani baadhi ya
maeneo mazao yamenyauka mashambani hivyo kutokana na ukosefu wa mvua za
kutosha.
“Jambo
la muhimu ni kupanga matumizi kwenye chakula tulicho nacho, tusiuze
ovyo,tunaelewa hali ya mvua haikuwa nzuri na siyo kwa Singida tu ni kwa mikoa
yote sasa tunakwenda kupanga foleni kwa nani,” alisema.
Dk.Mahenge
alisema kutokana na hali hii iliyopo ambayo inaonesha dalili za upungufu wa
chakula, wananchi wahakikishe wanalima mazao yanayoweza kustawi maeneo yenye
unyevunyevu.
“Ni
lazima tujiongeza mwenye kuku afuge, watu wanatoka Dar es Salaam kuja kununua
kuku Singida hizo hela ukizipata unanunua mahindi, tusiweke. Matumaini sana
kwamba tutaletewa chakula cha msaada,” alisema.
Alisema
kimsingi hali ya chakula katika dunia sio nzuri kwani hata nchi ambazo huwa
tunapata msaada wa chakula nao hakitoshi na hata mafuta ya kula hayawatoshi
pia.
“Kule
Ulaya wazungu shamba lao anazaliwa anakuwa mkubwa hawajawahi kuwa na ardhi,
hawajawahi kuona muhindi wala mgomba duka lake ni ‘Super Market’ akiingia
anakuta kuna magimbi na kila kitu, wao wameishi katika mazingira kama hayo,”
alisema.
Mkuu
wa Mkoa alisema ‘ super market’ ya mtu mweusi (mwafrika) iko shambani hivyo
watu wajiongeze maeneo ambako kuna mito kuna maji wapande mazao yanayostahimili
maji kidogo kama vile mihogo, viazi vitamu ili kuweza kuokoka na baa la njaa
linaloweza kujitokeza.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro, alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa kutokana na
wananchi wengi katika wilaya take kutovuna kabisa kukikosabishwa na ukosefu wa
mvua, serikali ya wilaya imeanza kufanga tathimini kupata idadi ya wananchi
ambao hawana chakula kabisa.
“Ndani
ya wiki hii tathimini itakwisha na nitakuandikia barua rasmi ya serikali ya
wilaya kuomba msaada wa mkoa ili tujue sisi wilaya tutaoata maasada gani kwenye
eneo la chakula.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi wakipokea kero kutoka kwa mwananchi aliyefika kwenye mkutano huo.
Wananchi wa Ikungi wakiwa wamejipanga foleni tayari kwa kutoa
kero zao kwa mkuu wa mkoa.
No comments
Post a Comment