Naibu Ruto nusura kumpiga kofi Rais Uhuru Kenyata
Mbunge wa Suna Mashariki nchni Kenya,
Junet Mohammed ametoa sauti ambayo ilimnasa Naibu Rais William Ruto akikiri
kwamba nusura ampige Rais Uhuru Kenyatta kofi kuhusu uamuzi wa Mahakama wa Upeo
kubatilisha uchaguzi wa urais wa 2017.
Mbunge huyo hakueleza chanzo cha sauti hiyo ambayo ilirekodiwa wakati wa mkutano wa faragha katika makazi ya DP Ruto huko Karen uliofanyika Ijumaa, Julai 1.
Yaliyomo kwenye rekodi hiyo
yaliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Daily Nation japo sauti hiyo
haikuwekwa wazi.
Hata hivyo, Junet alicheza kanda hiyo
kamili wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Azimio Raila Odinga huko Ndhiwa,
Homa Bay ambapo waliohudhuria walikuwa wametakiwa kuacha simu zao nje ya
chumba.
Katika kanda hiyo, Ruto anasikika
akicheka alipokuwa
akizungumza kuhusu yale Rais alikuwa
akifanya siku hiyo.
“Nilitoka hapa nikaenda Ikulu, sitaki
kusema nilipofika huko alikuwa anafanya nini maana sisi ni wazee (anacheka)
akaanza kunung’unika akisema hataki tena anataka kwenda kwa Ichaweri na kwamba
tumuache awe.”
“Nilimtazama na kumwambia kuwa wewe! Nivile nilikuwa tu namheshumu bure ningempiga kofi kisha tukaacha tukaondoka?” DP alisema.
Junet alidai kuwa rekodi hiyo
ilithibitisha kuwa nchi hii haitakuwa salama chini ya uongozi wa mtu ambaye
angekuwa na ujasiri wa kumpiga kofi rais aliye madarakani.
No comments
Post a Comment