NECTA yatangaza matokeo kidato cha sita
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) leo
Jumanne Julai 5, 2022 limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na
kusema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 99.87.
Akitangaza matokeo hayo visiwani Zanzibar leo
Kaimu Katibu wa Baraza Hilo, Athuman Amas amesema mwaka huu idadi ya ufaulu ni
asilimia 99.87 ikilinganishwa na asilimia 99.62 ya mwaka jana.
“Watahiniwa
93,136, sawa na asilimia 98.97 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 40,907 sawa
na wavulana waliofaulu ni 52, 229.
Ufaulu katika masomo ya Historia, Kiingereza,
Kifaransa, Kiarabu, Physics, Chemistry, Biology, Kilimo, Advanced Mathematics,
Economics, Accountancy, na Food/HumanNutrition umepanda ikilinganishwa na mwaka
2021.
Hata hivyo, NECTA imesema ufaulu wa Masomo
mengine yakiwemo General Studies, Geography na Basic Applied Mathematics (BAM)
umeshuka.

No comments
Post a Comment