Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Wawakilishi wa Bodi ya
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSSF) katika ofisi ndogo
za Wizara leo tarehe 6 Julai 2022 jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo
hayo Waziri Mulamula amewahakikishia Wawakilishi hao kuwa
Serikali inaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili
kukuza sekta za uzalishaji kwa maslahi mapana
ya Taifa.
‘’ Wizara kupitia
Balozi zetu nje imeendelea kuhakikisha fursa mbalimbali
zinazopatikana nchini zinatangazwa katika
maeneo ya uwakilishi
ili kuzihakikishia sekta hizo mageuzi makubwa ya kiuchumi” alisema Balozi
Mulamula.
Naye Mwenyekiti wa
Bodi ya TPSF, Bi. Angelina Ngalula pamoja na wajumbe
alioambatana nao wameipongeza na
kuishukuru Serikali
ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka
mkazo wa kuinua sekta binafsi.
Akifafanua Bi.
Ngalula ameeleza juu ya uwepo wa mafanikio katika sekta za biashara,
Utalii, uwekezaji, kilimo, madini,
huduma, uchukuzi na
usafirishaji na ujenzi.
“Sisi sekta binafsi
tunaishukuru Serikali yetu kwa kuboresha mazingira ya biashara,
sasa tunashuhudia mipaka inafunguka sambamba na ongezeko la watalii kupitia
jitihada za makusudi
zinazofanyika katika
kuitangaza filamu ya “Tanzania the Royal Tour” alisema Bi. Ngalula
Aidha, akafafanua
matokeo yaliyopatikana kupitia ziara za Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwamba kupitia
ziara hizo mikutano na makongamano ya
biashara yalifanyika
katika nchi mbalimbali na yamesaidia kupatikana kwa washirika wa
kibiashara kutoka mataifa hayo.
Kupitia mazungumzo
hayo Waziri Mulamula na Wawakilishi wa Bodi ya Taasisi ya Sekta
Binafsi, wamekubaliana kuanzisha timu maalum ya uratibu na ufuatiliaji wa
masuala mbalimbali ya
kimkakati kitaifa,
kwa lengo la kuimarisha na kukuza diplomasia ya uchumi nchini.
Waziri Mulamula akizungumza na Wawakilishi wa Bodi ya TPSF kutoka katika Sekta za Huduma, Sekta Umma, Sekta ya Wenye Viwanda Vidogo,Sekta ya Wafanyabiashara Wanawake, Sekta ya Uhandisi na Ujenzi, na ulioambatana, Uongozi wa TPSF uliokuwa umeambatana na Bi. Ngalula.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga akifafanua jambo katika mazungumzo hayo
Balozi Mulamula akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Bi. Ngalula vitabu vya Diplomasia ya Uchumi.
No comments
Post a Comment