Mtibwa Sugar wagoma kutoka ligi Kuu Bara, TZ Prisons bado wana mzigo
Licha
ya kupoteza kwa 1-0 kwenye Uwanja wa Manungu Complex katika mchezo wa Mkondo wa
Pili wa Hatua ya Mtoano ‘Play Off’ dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza
Tanzania Prisons, Klabu ya Mtibwa Sugar imesalia Ligi Kuu Tanzani Bara.
Mtibwa
Sugar imesalia katika hatua hiyo, kufuatia ushindi wa 3-1 iliyouvumna katika
mchezo wa Mkondo wa Kwanza Hatua ya Mtoano ‘Play Off’ uliopigwa Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya Jumapili (Julai 03).
Bao pekee la Tanzania Prisons katika mchezo wa mkondo wa pili lilifungwa na Mshambuliaji Mudathir Abdallah, ambalo halikutosha kuharibu mipango ya Mtibwa Sugar iliyoibuka na ushindi wa jumla wa 3-2.
Hivyo
Tanzania Prisons inaendelea na mpango wa kusaka nafasi ya kurejea Ligi Kuu
Tanzania Bara kwa kucheza mchezo mwingine wa Mtoano ‘Play Off’ dhidi ya JKT
Tanzania inayotokea Ligi Daraja la Kwanza.
Mchezo
wa raundi ya Kwanza kwa Miamba hiyo utachezwa Jumamosi (Julai 09), Uwanja wa
Jenerali Isamuyo jijini Dar es salaam, kabla ya kucheza mchezo wa raundi ya
Pili Jumatano (Julai 13) katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mshindi
wa jumla katika mchezo huo atapanda Daraja na kucheza Ligi Kuu Msimu wa 2022/23
ambao utaanza rasmi Agust 13.
No comments
Post a Comment