Ahmed Ally amnadi Suma Mwaitenda
Meneja
wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amejitokeza hadharani na
kumpigia Kampeni Mgombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Young Africans Suma
Mwaitenda.
Mwaitenda
amejitosa kuwania nafasi hiyo, ikiwa ni mara yake ya pili kuingia kwenye
Uchaguzi Mkuu wa Young Africans, akifanya hivyo miaka minne iliyopita kwa
kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Ahmed
Ally amempigia Kampeni Mgombea huyo kwa kuwataka Wanachama wa Young Africans
kumuamini, kama Simba SC ilivyomuamini Mwanamke Barbara Gonzalez kwa kumpa
nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu ‘CEO’.
Ahmed
ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe wa kumpigia kampeni Suma
Mwaitenda ambaye amedai ni Rafiki yake wa karibu.
Wapo
Wanawake wachache wenye uthubutu wa kuongoza vilabu vikubwa
Rafiki
yangu binafsi @sumamwaitenda anahitaji ridhaa kubwa ya kuwa makamu wa Rais ni
nafasi kubwaa mnoo lakini sina mashaka na ubora wake na uwezo wake
Kila
la @sumamwaitenda kwa maslahi ya mpira wa miguuu
No comments
Post a Comment