Serikali Tabora kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto
Serikali Mkoani
Tabora imesema itahikikisha inapambana vikali kuzuia vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa
watoto wadogo ndani ya mkoa huo.

Mkuu wa wilaya ya Nzega kamishina msaidizi wa polisi Advera Bulimba akitoa zawadi kwa mmoja ya wanafunzi walionda tuzo ya uandishi wa Insha iliyohusu mimba na ndoa za utotoni
Hayo yamezungumzwa
ikiwa tatizo la ukatili wa kijinsia ,mimba na ndoa za utotoni
likitajwa kushika kasi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tabora ambapo
serikali imetaja kuongeza makali ya kusimamia sheria kwa wale wanaokamatwa na
tuhuma za kuvunja matakwa ya haki za watoto .
Mkuu wa wilaya
ya Nzega kamishina msaidizi wa polisi
Advera Bulimba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Tabora balozi Dkt. Batilda Buriani katika hafla fupi
ya kuwapongeza wanafunzi walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu
ukatili na kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Alisema
kwamba serikali haina lelemama na wale ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya
hovyo kwa watoto.
Mkuu
huyo wa wilaya aliendelea kusema kwamba serikali ya mkoa wa Tabora
itapingana kuhakikisha Ukatili dhidi matendo ya ubakaji,
ulawiti, utumikishwaji wa watoto, kunyimwa haki ya elimu, vipigo, kutopatiwa
mahitaji ya msingi au kutelekezwa pale wazazi wanapotengana, kudhulumiwa
mirathi na walezi vinakomeshwa ili kuweza kumlinda motto huyo.
“Wazazi
wanapofariki,watoto wa kike kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo na mimba za
utotoni jambo ambalo linakera sana kwani sio haki kwa mtoto kupitria madhira
hayo” alisema Advera Bulimba
ACP
Advera Bulimba alisema kwamba serikali itaendelea
kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo
ili kuhakikisha adhma ya kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili
inatekelezeka kwa vitendo.
Akizungumza
kwa niaba ya mkurungezi wa shirika la World Vision Esther Mongi alisema kwamba
Mtoto aliyefanyiwa vitendo kikatili anaweza kupata madhara ya
kisaikolojia, kimwili na kitabia, pia kuathiri mwenendo mzima wa malezi na
makuzi, kujifunza na mahusiano yake na jamii hapo baadaye atakapokuwa mtu
mzima kwa kuendelea kuamini kuwa ukatili ni sehemu ya maisha.
Alisema kwamba
Vitendo vya ukiukwaji wa haki za Watoto hufanywa na wazazi, walezi, ndugu
waliopo katika familia, Watoto kwa Watoto, wanajamii kwa kuwapatia watoto kazi
ngumu na kuwafanyia ukatili kutokana na umaskini .
Aliendelea
kusema kwamba baadhi ya watendaji wa Serikali, wafanyakazi katika
mashirika yasiyokuwa ya serikali, na wamiliki wa migodi na Wafanyabiashara.
Alisisitiza
kwamba shirika la World Vision litaendelea kupambana na mila na desturi,
mabadiliko ya sayansi na teknolojia navyo vimeendelea kuwa ni visababishi vya
matendo ya ukatili kwa Watoto.
Aidha
kaimu mkurungezi huyo alisema kwamba shirika la World Vision
Esther Mongi litaendelea kuwajengea uwezo watoto ili waweze
kujiamini na kujitambua ikiwa hatua ya kukabiliana na tatizo
la mimba na ndoa za utotoni .
Alisema
kwamba shirika hilo linaendelea kuratibu mashindano
ya uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za
msingi ambapo katika Mkoa wa Tabora washindi
wamepewa zawadi za baiskeli na fedha tasilimu
huku mshindi wa kwanza kwa mkoa wa Tabora
akitarajiwa hivi karibuni kwenda kushiriki mashindano
hayo kitaifa Mkoani Dodoma.
Afisa maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Robert Mwanga alisema jamii inatakiwa kuwa sehemu ya kuwalinda watoto huku watoto wenyewe wakiombwa kuwa ni sehemu ya kutoa taarifa pale wanapokumbana na viashiria vya uvunjifu wa haki zao.

Mkuu wa wilaya ya Nzega kamishina msaidizi wa polisi Advera Bulimba akitoa zawadi kwa mmoja ya wanafunzi walionda tuzo ya uandishi wa Insha iliyohusu mimba na ndoa za utotoni
No comments
Post a Comment