Simba SC yatamba kuisimamisha Afrika kwenye dirisha la usajili
Klabu ya
Simba SC huenda ikaanza kutangaza wachezaji waliowasajili katika kipindi hiki
cha Dirisha la Usajili, kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na Michuano ya
Kimataifa msimu wa 2022/23.
Simba
SC imekua kimya katika usajili, baada ya kutambulisha Mshambuliaji kutoka
nchini Zambia Moses Phiri mwezi uliopita, akitokea Zanaco FC.
Simba
SC imeweka ujumbe kwenye kusara zake za mitandao ya kijamii, ambao unaonyesha
namna walivyojiandaa kutangaza orodha ya wachezaji waliosajiliwa.
Ujumbe huo unasomeka “Mwaka
huu utambulisho wetu sio tena wa kusimamisha nchi bali bara zima la
Afrika ”

No comments
Post a Comment