Wachimbaji Bahi waagizwa kulipa wafanyakazi wao
Waziri
wa Madini Dkt. Doto Biteko, ametoa wiki moja kwa wachimbaji wa madini ya Chuma
wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma kulipa madeni wanayodaiwa na wananchi katika
migodi hiyo kwa wanaofanya kazi ya kuponda madini hayo.
Agizo
hilo amelitoa wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Asanje mara baada ya
kutembelea maeneo ya wachimbaji wa chuma na kupokea malalamiko.
Dkt.Biteko,
amemwelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma kusimamia agizo hilo kwa
kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda ili wanachi hao wa
Asanje walipwe fedha zao wanazowadai wawekezaji hao.
“Mhe.
Mkuu wa wilaya, kama kuna mtu atakuwa hajalipwa hadi jumatatu Afisa Madini
unasimamisha mgodi huo mara moja bila masharti yoyote, uandike kabisa kwa
maelekekeao ya Waziri nasimamisha,” amesisitiza Dkt. Biteko.
Aidha,
amewataka wachimbaji wa madini na wawekezaji katika Sekta ya Madini kuhakikisha
wanashirikisha wananchi katika mipango yao ya uwekezaji kabla hawajawekeza
kwenye miradi hiyo ili kupunguza malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara.
Amesema,
ushirikishwaji utasaidia kujua vipaumbele vya wanachi ili iwe rahisi kwa
utekelezaji.
“Nataka
niwaambieni wenye leseni, leseni hizi mmepewa kwa niaba ya Watanzania wengine.
Kwa kuwa tumewapa wenzetu leseni ya kuchimba matarajio ya Serikali ni kwamba
hawawezi kugeuka tena kuwa kero kwa watu ambao wako maeneo ya kuchimba,”
amesema.
Naye,
Mbunge wa Jimbo la Bahi, Kenneth Nolo amesema, ziara ya Dkt. Biteko katika
Kijiji cha Asanje kusikiliza malalamiko ya wanachi hao, imekuwa na manufaa kwa
wananchi na matarajio makubwa katika shughuli za uchimbaji madini.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Munkunda amemshukuru Dkt. Biteko kwa kuweza kufika na kusikiliza changamoto za wananchi hao kwani ilikuwa ni kiu kubwa ya kuweza kufikisha malalamiko yao kwake.Wilaya ya Bahi yanapatikana madini mbalimbali yakiwemo dhahabu, chuma na madini ujenzi.



No comments
Post a Comment