Tanzania kusaini mikataba ya ushirikiano kufundisha Kiswahili nchini Afrika Kusini
Tanzania na Afrika Kusini zinatarajia kusaini mkataba
wa makubaliano ya ushirikiano katika maswala ya elimu siku ya
Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Duniani ambayo kitaifa
yatafanyika Jijini Dar es salaam, julai 7 mwaka huu.
Kati ya makubaliano hayo yatakayowezesha kuimarisha
ushirikaino kwa nchi hizo mbili ni pamoja na Tanzania kuisaidia Afrika Kusini
kufundisha lugha ya Kiswahili.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof
Adolf Mkenda ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri
wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini Mhe Matsie Angelina Motshekga katika ukumbi
wa kimataifa wa mikutano (JNICC) Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Waziri
Mkenda amesema kuwa mkataba huo wa makubaliano unasainiwa ikiwa ni kutekeleza
ahadi ya viongozi wakuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Samia Suluhu Hassan na Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa waliyoitoa ya
kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu.
Waziri Mkenda amesema kuwa mara baada ya kusainiwa
makubaliano hayo viongozi wakuu watakutana kwa ajili ya kuweka mpango kazi wa
utekelezaji ili isiwe ni makubaliano pekee pasipo utekelezaji wake.
Waziri huyo wa Elimu wa Afrika Kusini anatazamiwa kutembelea shule ya msingi ya Uhuru Mchanganyiko ili kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula pamoja na kukutana na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mohamed Mussa.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika
Kusini Mhe Matsie Angelina Motshekga amesema kuwa Afrika Kusini ina mtazamo
mkubwa na Tanzania kubadilishana uzoefu katika udhamini wa mafunzo
(Scholarship), kufanya kazi kwa pamoja na kubadilishana uzoefu katika sekta
nzima ya elimu.
Mhe Motshekga amesema kuwa amekuja kusaini
makubaliano hayo kwani yatakuwa muhimu na yenye tija kwa Tanzania pamoja na
wananchi wa Afrika Kusini ambao wanaipenda na kuithamini lugha ya Kiswahili.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja
Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi amesema kuwa baada ya kusainiwa kwa
makubaliano hayo bado Tanzania itaendelea kutumia fursa za kufundisha Kiswahili
katika maeneo mengi
No comments
Post a Comment