Taarifa kutoka jeshi la polisi mkoa wa Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu.
Tukio la kwanza.
Ndugu waandishi wa
Habari, tarehe 05.07.2022 majira ya 12:30hrs mchana huko eneo la pamba road
sokoni Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza, Jeshi la polisi lilimkamata Said
Furaha Miaka 31, Msukuma, Mkazi wa Nundu, Mfanya biashara, kwa kosa la
kupatikana na jezi bandia dazani 145 zenye nembo ya club ya simba zinazo
milikiwa na kampuni ya VUNJA BEI na jezi dazani 151 zenye nembo ya Club ya
Yanga zinazo milikiwa na kampuni ya GSM, kitendo ambacho nikinyume na sheria.
Awali Jeshi la
Polisi lilipata taarifa toka kwa afisa masoko wa kampuni ya GSM na VUNJA BEI
kuwa hapa Jijini Mwanza kuna mfanya biashara anaesambaza na kuuza jezi bandia.
Baada ya taarifa hizo ufatiliaji wa kina na haraka ulifanyika na kufanikiwa
kumkamata mtuhumiwa tajwa hapo juu akiwa na jumla ya dazani 296 bandia za club
ya Simba na Yanga dukani kwake.
Aidha, Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mwanza linaendelea na upelelezi wa kina kuhusiana na shauri hili
ili kuweza kubaini mtandao mzima wa wahusika wote wanao tengeneza, kuagiza na
kuingiza nchini bidhaa hizo bandia, ambapo inapelekea wadhamini wa club hizo
kukosa mapato. Upelelezi wa shauri hili unakamilishwa mara moja na mtuhumiwa
atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo.
Tukio la Pili.
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu wawili ambao ni Omary Lucas, Miaka 48, Mkazi
wa Buhongwa ambaye ni mume wa marehemu na Amos Lucas , Miaka 29, Mlinzi,
Mkazi wa Isabenda kwa tuhuma za kosa la mauaji ya Elizabeth Lusana, Miaka 61,
Mkazi wa mtaa wa Kagera, kata ya Lwanhima, Wilaya ya Nayamagana aliyeuawa mnamo
tearehe 11.07.2022 majira ya 01:00hrs usiku kwa kukatwa na kitu chenye ncha
kali maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Uchunguzi wa awali
umebaini wanandoa hao walikuwa na ugomvi uliotokana wivu wa kimapenzi ambapo
mwanaume alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano yasiofaa nje ya ndoa
ulio pelekea mauaji hayo. Mtuhumiwa baadaya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na
kwenda kujificha Mkoani Tabora kwa Amos Lucas, lakini ufatiliaji wa Polisi
uliweza kubaini mahali alipo na kuwakamata yeye pamoja na mtu aliyemficha.
Tukio la tatu.
Ndugu wanahabari,
tarehe 12.07.2022 majira ya 19:19hrs usiku huko mtaa wa Nyabulogoya, kata ya
Nyegezi, Wilaya ya Nyamagana, mtoto mwenye umri wa miaka 5 na nusu aitwaye Ally
Sipendeki, mwanafunzi wa shule ya chekechea ya ST. Benedict English Medium
–Nyegezi, alifariki dunia baada ya kuungua na moto kutokana na ajali ya moto
ulionguza nyumba ya Pastory Nestory, miaka 70, mwalimu mstaafu wa
Nyabulogoya.
Moto huo pia
umeteketeza mali za wapangaji watatu wa nyumba hiyo ambazo thamani yake bado
kufahamika. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Jeshi la Zima
Moto na Uokoaji na vyombo vingine vya usalama lilifika kwa haraka eneo la tukio
na kuanza kuzima moto huo kwa kushirikiana na wananchi kabla ya kuleta madhara
makubwa.
Chanzo cha moto huo
bado kinachunguzwa kwa kushirikiana na idara zinazo husika. Mwili wa marehemu
umehifadhiwa Hospitali ya rufaa ya Bugando kusubiri uchunguzi wa daktari, baada
ya uchunguzi kukamilika utakabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mwanza linawashukuru wananchi kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika
kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Jeshi linazidi kutoa onyo kwa watu
wenye kujihusisha na vitendo vya kihalifu kuwa hawatoweza kukwepa mkono wa
sheria kwa haliyoyote ile.
Imetolewa na;
Ramadhani H.
Ng’anzi- SACP.
Kamanda wa Polisi
(M) Mwanza.
No comments
Post a Comment