TCRA yateta na watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao kanda ya ziwa
Lengo la kikao hicho ni kujadiliana kuhusu mambo mbalimbali hususani uzingatiaji wa masharti ya leseni, kanuni na sheria katika utoaji wa maudhui ya mtandaoni pamoja na uelewa juu ya marekebisho ya kanuni za maudhui mtandao.
Kikao hicho kinalenga kuongeza uelewa kuhusu marejeo pamoja na kanuni za maudhui mtandaoni, kuongeza uhusiano baina ya TCRA na wenye leseni za mtandao pamoja na kupunguza makosa yanayojitokeza wakati wa uwasilishaji wa maudhui mtandao yanayotokana na ukiukwaji wa kanuni hizo.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati akifungua kikao kazi na Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Mwanza Press Club, Edwin Soko akitoa mada kuhusu Vitisho vya Kimtandao na Ulinzi wa waandishi wa habari Mtandaoni kwenye kikao kazi cha TCRA na Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa
Mwenyekiti Mstaafu wa Mwanza Press Club, Deus Bugaywa akitoa mada kuhusu Maadili kwa vyombo vya habari vya Kimtandao
No comments
Post a Comment