Wanafunzi waomba kuishi shuleni na watoto wao
Kutokana na kukosa umakini darasani, baadhi ya
wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatisha masomo kutokana na ujauzito,
wameomba kujengewa hosteli zitakazowasaidia kuwa karibu na watoto wao.
Ombi hilo limetolewa kwa Makamu wa Rais wa
Benki ya Dunia (WB), Dkt. Victoria Kwakwa katika ziara yake aliyoifanya Shule
ya Msingi Turiani kufuatilia utekelezaji wa mradi wa kuwarejesha masomoni
wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na matatizo mbalimbali, ikiwamo
ujauzito.
Mbali na ombi hilo, pia wameomba kuboreshewa
miundombinu ya kujifunzia ili waondokane na mfumo wa kusoma kwa nadharia hali
itakayowasaidia kumudu ushindani wa kusoma na kuelewa.
“Kwa sababu tunatoka mbali, tunafika nyumbani
tumechoka na tunakosa muda wa kusoma tunaomab kujengewa hostel hii itatusaidia
kuwa karibu na watoto wetu kwa sababu wakati mwingine tunakosa umakini darasani
kutokana na mazingira tuliyowaacha watoto wetu,” alisema mmoja wa Wanafunzi
hao.
Hata hivyo, Dkt. Victoria amesema wataendelea
kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kufanya maboresho yatakayowezesha wanafunzi
wengi kurudi darasani na kuendelea na masomo yao.
No comments
Post a Comment