Majaji wa mahakama ya Juu nchini Kenya, wanaendelea kusikiliza ushahidi na mawasilisho ya upande wa mgombeaji wa muungano wa Azimio la Umoja
Majaji wa mahakama ya Juu nchini Kenya, wanaendelea kusikiliza ushahidi na mawasilisho ya upande wa mgombeaji wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga, kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.
Wakili wa Raila, James Orengo tayari amewasilisha stakabadhi za ushahidi kuonyesha kwamba William Ruto hakupata asilimia 50+1 ya kura zilizopigwa kama ilivyotangazwa na mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC), Wafula Chebukati
Amesema, kulikuwa na tofauti ya idadi ya wapiga kura ambao mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza kwamba walijitokeza kupiga kura hivyo kuleta sintofahamu katika ujumlishaji wa matokeo ya ujumla.
Orengo, pia amedai kulikuwa na mkanganyiko wa kura kuondolewa kutoka kwa Raila na kuongezwa kwa mpinzani wake William Ruto, ili kuhakikisha kwamba anaafikia kiasi cha idadi ya kura zinazohitajika na kutangazwa mshindi.
No comments
Post a Comment