Mawaziri wa ulinzi wa EU wakubalianakuandaa utoaji mafunzo kwa wanajeshi .
Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana hii leo kuanza maandalizi ya mpango wa jumuiya hiyo wa kutowa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine. Makubaliano hayo yamefikiwa kwenye mkutano usiokuwa rasmi mjini Prague.
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell aliyeongoza mkutano huo pamoja na uongozi wa jamhuri ya Czech ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya amesema wanapaswa kuhakikisha kwamba juhudi hizo zitakuwa na uthabiti kwasababu vita vya Ukraine sio vita tu, bali pia vinahusu namna vinavyoendeshwa na aina ya mafunzo ya wanajeshi.
Hakuna maelezo mengi yaliyotolewa kuhusu kilichokubalika lakini Josep Borrell amesema wanajeshi wa Ukraine wanaopambana na vikosi vya Urusi wanapaswa kupewa mafunzo katika nchi za karibu ndani ya Umoja wa Ulaya.
No comments
Post a Comment