Urusi Kuingia Makubaliano na Taliban Kupeleka Bidhaa Afghanistan, Baada ya Nchi Hizo Kuwekewa Vikwazo vya Kimataifa
MUDA sio mrefu kutokea sasa Urusi itaingia makubaliano na uongozi wa Taliban nchini Afghanistan juu ya uagizaji wa ngano,mafuta na gesi kutoka Urusi kwenda nchini Afghanistan.
Msemaji wa wizara ya uchumi ya Afghanistan amethibitisha kuwa wawakilishi wa serikali yao wapo Urusi kukamilisha makubaliano hayo na ameongezea kwa kusema ya kwamba wakati huu wapo katika mchakato wa kutafuta namna ya kufanya malipo ya bidhaa hizo wanazoagiza ikiwemo ngano, mafuta na gesi.
Taliban wamepitia changamoto hii ya kutafuta njia mbadala ya malipo kufuatia kutotambuliwa na jamii ya kimataifa, hivyo benki za kimataifa kushindwa kufanya biashara na benki za Afghanistan.
Vilevile vikwazo vilivyowekwa kwa nchi zote mbili Urusi na Afghanistan vimechangia kutia ugumu kwa kufanyika kwa biashara hiyo kati nchi hizo mbili.
Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.
No comments
Post a Comment