Header Ads

Header ADS

Matteo Salvini asema vikwazo ilivyowekewa Urusi havifanyi kazi


 

Cernobbio, ItaliaKiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia nchini Italia Matteo Salvini, amezua gumzo nchini humo baada ya kusema kuwa vikwazo ilivyowekewa Urusi na mataifa ya Magharibi kufuatia taifa hilo kuiingilia kijeshi Ukraine havifanyi kazi. 
Kupanda maradufu kwa bei ya nishati ya gesi tangu kuanza kwa vita vya Urusi na Ukraine kumeyumbisha uchumi wa mataifa kadhaa ya Ulaya ambayo kabla ya vita yalikuwa tegemezi wa gesi kutoka Urusi.   
Salvini amesema miezi kadhaa imepita na watu wanaendelea kulipa gharama ya mara mbili hadi nne ya bei ya nishati kuliko walivyokuwa wakilipa hapo mwanzo huku akisema vita bado vipo na Urusi inaendelea kunufaika. Matteo Salvini amesisitiza kuwa ni muhimu kufikiria tena mikakati ya kuokoa ajira na biashara. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania cMhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Abiria na Wananchi mbalimbali aliosafiri nao kwa Meli ya  M.V Kilimanjaro 4 alipokuwa akiondoka katika Bandari ya Malindi Zanzibar akielekea Jijini Dar es Salaam  tarehe 05 Septemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu kwenye Meli ya Kilimanjaro 4 alipokuwa akiondoka katika Bandari ya Malindi Zanzibar akielekea Jijini Dar es Salaam  tarehe 05 Septemba, 2022

No comments

Powered by Blogger.