Header Ads

Header ADS

Simba Queens yakabidhiwa basi jipya

 Kampuni ya uuzaji wa magari ya Africarriers imetoa basi kwa Timu ya Wanawake ya Simba Queens kwa ajili ya usafiri wa ndani ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba.

Africarriers ambayo imekua sehemu ya wadhamini wa Simba SC tangu msimu uliopita imefanya hivyo ikiwa ni hatua ya kuendeleza makubaliano waliyoingia na Uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu Msimbazi jijini Dar es salaam.

Hafla ya kukabidhi basi hilo aina Eicher imefanyika leo Ijumaa (Septemba 02), katika ofisi za Africarriers zilizopo Barabara ya Pugu na kuhudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez, Kocha Mkuu wa Simba Queens Sebastine Nkoma na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi










No comments

Powered by Blogger.