Header Ads

Header ADS

Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss ameahidi kuwalinda Wananchi wake

Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss ameahidi kuwalinda Wananchi wake kutokana na athari mbaya za kupanda kwa gharama za nishati na kutekeleza “mpango wa ujasiri” wa kufufua uchumi.
Truss, ameyasema hayo kupitia hotuba yake kwa Taifa hilo ikiwa ni siku ya kwanza akiwa kazini, katika cheo cha Uwaziri Mkuu wa Uingereza, na kuahidi kushughulikia kero mbalimbali za kitaifa.
Amesema, “Kama dhoruba inaweza kuwa kali, najua kwamba watu wa Uingereza wana nguvu zaidi na kuhusu mshtuko wa bei ya nishati, ukuaji wa polepole na mfumuko wa bei wa tarakimu mbili nina uhakika wa kuukabili na kuleta ahueni.” 
Wataalam walio wengi, wanaonya kuwa mamilioni ya Waingereza wanaweza kukabiliwa na ufukara kutokana na bili za nishati ambazo zinaweza kupaa hadi asilimia 80 mwezi Oktoba, ambapo Truss anatarajiwa kuingiliaji kati masoko ya nishati.
Maelezo hayo, ambayo yanaweza kujumuisha kupunguza bei ya nishati kwa gharama kwa serikali ya dola bilioni 100 au zaidi, huenda yakatangazwa wiki hii.
Truss, anakuwa Waziri Mkuu wa nne wa Uingereza katika kipindi cha miaka sita, ambapo leo amejibu maswali ya wabunge, akiwemo kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Keir Starmer.
Mapema wiki hii, chama cha Labour kiliunganisha uongozi muhimu katika kura za maoni, na kufanya uwepo wa hatari kwa Truss anakayepokea uungwaji mkono mkubwa anapochukua mamlaka.
Baraza jipya la mawaziri la Truss, pia linatarajia kuwa na watu waliomuunga mkono mpinzani wake, Rishi Sunak ambaye walishindana katika kampeni iliyojaa tofauti za kikabila na kijinsia za wagombea wake.


No comments

Powered by Blogger.