Header Ads

Header ADS

Deodatus Balile ,ashauri vifungu vya sheria zinazowabana wanahabari virekebishwe

 

Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) ndugu Deodatus Balile ameshauri baadhi ya sheria za habari zinawabana waandishi wa habari na kushidwa kufanya kazi kwa weledi lakini pia zinawabana na kushidwa kutetea haki na maslahi yao huku akitolea mfano vyuo vingi vya Africa vinafundisha waandishi wa habari kutetea jamii huku akisema katika mafunzo hayo hamna sehemu inamwambia mwandishi kwamba naye ni mmoja wa kundi linalotakiwa kutetewa kitu ambacho kinafanya waandishi wengi kushidwa kujieleza kuhusu matatizo wanayokutana nayo katika kazi zao.
Baadhi ya taasisi zinadai kutetea haki za waandishi wa habari lakini hawajui chochote kuhusu changamoto hizo ndio maana sisi Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) tukasema tuanze kutetea haki na maslahi ya waandishi wa habari , Sisi ndio tunafanya kazi za habari ndio tunajua changamoto tunazokutana nazo hivyo sisi ndio tunaweza kujieleza na kutetea haki zetu ili duniani itambue na tupate namna ya kutatua changamoto hizo,
Amesema.
Ndugu Deodatus ameendelea kusema baadhi ya vifungu vya sheria ya habari vinawabana waandishi hivyo wapo kwenye michakato kuwaomba watunga sheria ili vifungu hivyo vifanyiwe marekebisho au kubadilishwa hasa vile ambavyo vimekuwa kikwazo kwa kazi za wanahabari.
Aidha Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe De Boer akifungua kikao kazi hicho amepongeza Jukwaa la Wahariri TEF katika programu zao za kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kufanya kazi kwa weledi zaidi na ameongeza kuwa sema ubalozi wa Uholanzi uko tayari kusaidiaTEF katika mipango yake. 


No comments

Powered by Blogger.