Waziri wa Ukraine apendekeza Serikali kufuta uhusiano na Iran
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema anawasilisha pendekezo la kumtaka rais Volodymyr Zelensky afute uhusiano wa kidiplomasia na Iran kutokana na nchi hiyo kuipelekea silaha Urusi.
Kuleba ameyasema hayo, katika mkutano wa waandishi habari kuwa Serikali ya mjini Tehran inawajibika kikamilifu kwa uharibifu unaofanyika nchini Ukraine na kuongeza kwamba Kiev itatuma barua rasmi kwa Israel wa kuiomba iwapelekee haraka silaha za mashambulizi ya anga pamoja na kuipa ushirikiano katika hatua hiyo.
Tamko hilo la waziri wa mambo ya nje wa Ukraine limekuja wakati Rais Zelensky kwa upande mwingine akisema mashambulizi ya Urusi yaliyoanza wiki iliyopita yameharibu asilimia 30 ya vituo vya nguvu za umeme vya nchi hiyo, na kusababisha maeneo mengi ya Ukraine kuwa kizani.
Haya yanajiri wakati ambapo, Waziri wa mambo ya ndani nchini Ujerumani Nancy Faeser akimfuta kazi mkuu wake wa usalama wa kimtandao, baada ya vituo vingi vya habari kuripoti uwezekano wa kuwa na mawasiliano na watu wanaohusishwa kufungamana na vyombo vya usalama vya Urusi.
No comments
Post a Comment